Serikali imebaini kuwepo kwa vyuo vikuu vingi visivyo na sifa, hivyo
inakusudia kuvifuta lengo likiwa ni kuhakikisha inaimarisha kiwango cha
elimu inayotolewa kwa ngazi zote.
Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ameyasema hayo leo
(Jumatatu), wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa elimu
ya juu.
Amesema hayo yamebainika baada ya jopo la wataalamu kufanya uhakiki kwenye vyuo hivyo nchini.
“Lengo ni kuhakikisha wasomi wanaohitimu kwenye vyuo hivyo wanakuwa
wameiva kitaaluma, ili pia waweze kushiriki katika kuijenga Tanzania ya
viwanda,” amesema Profesa Ndalichako.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya vyuo vikuu nchini(TCU) Profesa Jacob
Mtabaji amesema wamejipanga kuhakikisha kwamba wanafanyakazi zao kwa
kusimamia mwongozo uliopo ili kuondoa uwepo wa vyuo vingi visivyo na
sifa.
Post a Comment