Mwanamke
mmoja aliyetajwa kwa jina la Lightness Kivuyo, mkazi wa Unga Limited
jijini Arusha, amefariki akiwa anaombewa nyumbani kwa mtu mmoja
anayejiita 'Nabii Rajabu'.
Dada wa marehemu, Juliana Kivuyo amesema kuwa ndugu yake alikuwa anaumwa na alipelekwa na mumewe kwa ajili ya maombezi kwa kwa Nabii Rajabu lakini alianguka na kufariki dunia wakati huduma ya maombezi ikiendelea
"Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya maombi "alisema
Anasema kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio alimkuta ndugu yake akiwa amelazwa kwenye kochi akiwa bila nguo na akiwa hana nyusi ambapo mwili wake ulikuwa umefunikwa na khanga na tayari alikuwa ameshafariki.
Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa katika Hospital ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo, walipokea mwili wa Lightness huku waliomleta wakidai kuwa wamemleta mgonjwa na sio marehemu, lakini baada ya kumpima waligundua alikuwa amefariki muda mrefu uliopita
Imeelezwa kuwa mume wa marehemu alisisitiza kuwa mke wake hajafa bali amezimia kwa muda mrefu
Kamanda wa polisi Mkoa wa, Charles Mkumbo alithibitisha tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na jeshi hilo.
Chanzo :HabariLeo