0

Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamini Sita amezindua Vikundi vya waendesha bodaboda katika kata ya Ndugumbi tandale jijini Dsm waliopewa mafunzo maalum na jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya Uporaji  kwa kutumia Pikipiki,Ujambazi pamoja na matukio ya uhalifu ili kukabiliana na matukio hayo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi.

Vikundi hivyo vilivyopatiwa mafunzo na jeshi la Polisi pia vimepatiwa vitambulisho maalum pamoja na mavazi ambayo yanatambulika katika kata hiyo ambayo imekuwa na matukio ya Uporaji kwa kutumia pikipiki nyakati za jioni hasa giza linapoingia.

Meya wa Kinondoni amesema mpango huo ambao umeonyesha mafanikio ya kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa kuwashirikisha waendesgha bodaboda unatarajiwa kuenezwa katika manispaa yote ya kinondoni kwa kuwapatia mafunzo maalum waendesha bodaboda.

Siku za hivi karibuni katika kata hiyo iliyopo tandale kumekuwa na ongezeko la matukio ya Uporaji wa kutumia bodaboda ambapo akina mama wengi wamejikuta wakiporwa na kujeruhiwa ,huku majambazi wanaotumia silaha na wakitumia pikipiki katika kufanikisha uhalifu wao.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top