Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, amewataka watendaji katika Sekta
ya Elimu na wa Serikali za Vijiji Mkoani humo kuhakikisha wanawasaka na
kuwachukulia hatua zinazostahili wale wote walio wapachika mimba watoto
wa shule na sekondari na kuwakatisha Masomo yao.
Zambi ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule za sekondari katika
Wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Lindi na kubaini katika kila shule
hizo kuna msichana au wasichana walioshindwa kufanya mtihani wa kidato
cha nne kutokana na kupata ujauzito.
Mkuu wa mkoa huyo alionyesha kutoridhishwa na mdondoko wa wanafunzi
mashuleni hasa baada ya kupata taarifa za baadhi ya walimu wakuu wa
shule hizo zikibainisha changamoto mbalimbali ikiwemo ya ujauzito.
Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa pia alijionea uchakavu wa
majengo na sakafu za madarasa ya shule zote za sekondari alizozitembea
ikiwemo, Nyengedi, Sekondari, Kiwalala pamoja na shule ya msingi
Mongomongo
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.