Na Mwandishi wetu
Mnada
wa tano wa korosho unaosimamiwa na kuratibiwa na chama kikuu cha
ushirika cha RUNALI, umesitishwa kutokana na mgomo wa wasafirishaji wa
zao hilo.
Meneja
wa chama hicho, Christopher Mwaya, alithibitisha kusitishwa mnada huo,
ambao ulitarajiwa kufanyika jumapili ya tarehe 13 mwezi huu. Meneja huyo
ambae chama chake kinasimamia na kuratibu kazi za vyama vya msingi vya
ushirika(AMCOS) vilivyopo katika wilaya za Nachingwea, Ruangwa na
Liwale, alisema mnada huo hautafanyika kama ilivyotarajiwa.
Kutokana
na kutopelekwa korosho kwenye ghala kuu kutoka kwenye maghala ya vyama
vya msingi. Mwaya alisema hali hiyo imesababishwa na wasafirishaji
wanaosafirisha zao hilo kutoka kwenye maghala ya vyama vya msingi kugoma
kuendelea na kazi hiyo.
"Mgomo
wa wasafirishaji ulianza tarehe tisa mwezi huu,tulitarajia kuingiza
kilo 99745000 ,hata hivyo hazikuletwa.Kwahiyo mnada hautafanyika kesho," alisema Mwaya.
Meneja huyo alisema wafanyabiashara hao (wasafirishaji) wanadai kuwa bei wanazolipwa kwa kazi hiyo ni ndogo.
"Walikutana
na mkuu wa wilaya wakazungumza wakaleta rate zao(viwango vya bei), hata
hivyo baadhi ya vyama vya msingi vinataka vifanyike kwanza vikao na
wakulima kabla ya kukubali mabadiliko na reti hazo," alifafanua.
Mmoja
wa wasafirishaji, ambae hakutaka jina lake litajwe kwa madai ya
kutopenda kujiingiza kwenye ugomvi na serikali, alikiri kuwa wameacha
kusafirisha kutokana na baadhi ya vyama kukiuka makubaliano, na vingine
vinataka viwalipe chini ya bei za msimu uliopita.
Mfanyabiashara
huyo alisema nijambo lisilokubalika wakati thamani ya shilingi inashuka
lakini wao walipwe chini ya bei za mwaka jana. Huku akibainisha kuwa
bei wanazotakiwa walipwe zitawasababishia hasara.
"Mimi binafsi siwezi kufanya kazi ambayo itanisababishia hasara, kwenye biashara siasa ziwekwe pembeni," alisema mfanyabiashara huyo.
Akizungumzia
suala hilo, mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango, alisema
kulikuwa na kukosekana makubaliano baina ya wasafirishaji na vyama vya
msingi, ambavyo ndivyo venye haki na jukumu la kusafirisha korosho za
wakulima kutoka kwenye maghala ya vyama hivyo kwenda kwenye maghala
maalum yanayotumika kuhifadhia na kuchukuliwa na wanunuzi.
Mkuu
huyo wa wilaya, ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama(w), alisema suala hilo lilifikishwa ofisini kwake na
limeshugulikiwa kikamilifu. Bali kuna wafanyabiashara wenye tamaa baada
ya kuona bei ya zao hilo ni mzuri mwaka huu.
Hata
hivyo wapo wasafirishaji wanaendelea kusafirisha. Alisema lengo la
serikali ni kuona wakulima wananufaika na kazi yao halali. Kwahiyo
haiwezi kutishwa na watu wachache, wenye tamaa na wanaofanya kazi kwa
mazoea.
"Mnada utafanyika jumatano ijayo baada ya kusitishwa wiki hii, wakulima wasiwe na hofu kila kitu kitakwenda vizuri," alisema.
Tangu
kuanza ununuzi wa zao hilo linazalishwa kwa wingi katika mikoa ya
Lindi na Mtwara, msimu wa 2016/2017, kwa minada minne iliyofanyika.
Jumla ya kilo 10,170,438 zimeuzwa.
Post a Comment