Leo November 11 2016 Kesi ya
Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema ambaye anatuhumiwa kwa uchochezi
imeendelea katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha ambapo Mbunge Lema
amerudishwa rumande baada ya upande wa Jamhuri kutoa hoja za kukata
rufaa iliyopelekea Lema kukosa dhamana.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo
Desdery Kamugisha alikuwa amefikia hatua ya kutoa dhamana lakini upande
wa Jamhuri ulileta hoja hiyo ambapo Hakimu alikubaliana na kusitisha
dhamana hiyo hadi pale upande wa Jamhuri utakapokata rufaa.
Wakili wa CHADEMA Shedrack Mfinanga
amesema baada ya hakimu kutoa uamuzi huo wataendelea kusubiri na
kufuatilia ili waweze kuamua kuhusiana na hatua watakazochukua juu ya
rufaa hiyo.
Post a Comment