0





Kapteni wa timu ya New generation,Weusu Mbala akipiga basi katika hatua ya kusaka ushindi lakini harakati hizo hazikuweza kuzaa matunda kwenye mchezo huo mpaka dakika 90 zinakamilika waliambulia kichapo cha mabao 2-1.

Novemba 18 katika mchezo wa kukata na shoka ligi daraja la nne (KUCHAUKA CUP 2016) kulikuwa na mchezo kati ya timu ya New generation dhidi ya Likongowele fc matoke ya mchezo huo timu ya Likongowele fc iliweza kuilaza New generation kwa magoli 2-1.

Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi,timu ya New generation ilionekana ikicheza kwa kuizarau timu ya Likongowele fc lakini hawakuamini kilichotea baada ya kufungwa magoli 2 bila katika kipindi cha kwanza mpaka dakika 45 za mapumziko.

Magoli ya timu ya Likongowele fc yalifungwa na mchezaji mmoja Ima Mpesugwe namo dakika ya 29 na goli la pili alitikisa nyavu dakika ya 39 na goli la kufutia machozo la New generation likifungwa na Mawazo Kiwima baada ya kupokea basi na kupiga kichwa dakika ya 47.

Novemba 21 kutakuwa ndio mwisho wa mashindano haya ambapo kutakuwa na mchezo mmoja kati ya timu ya Black star ikiwakaribisha timu ya Nangando fc mchezo utakaopigwa uwanja wa halmashauri ya Liwale majira ya jioni.

Post a Comment

 
Top