0

Kuna jambo kubwa sana ambalo linaweza kubadili maisha yako ndani ya muda mfupi, ambalo siku ya leo ni vyema kulifahamu, na si kulifahamu tu bali kuamua kulichukua jambo hili na kulifanya libadili maisha na jambo lenyewe si jingine bali ni mtazamo ulionao.

Mtazamo ni vile ambavyo unaamini huenda ikawa ni katika fikra chanya au fikra hasi. Lakini katika makala haya nitazungumzia umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya, kwani mitazamo ya watu ndio ambayo humueleza kwa undani zaidi ni kwa njisi gani mtu alivyo kutokana na vitu ambavyo anavyovifanya na asivyovifanya.

Na jambo hilo huleta tofauti uliyopo kati ya walinacho na wasionacho, na tofauti hiyo ni kwamba waliofanikiwa wao wanaamini ya kwamba katika dunia hii hakuna kisichowezekana ila watu ambao hawajafanikiwa wao huamini ya kwamba mambo  mengine hayawezekani hii ni kutokana wao hukata tamaa mapema zaidi kabla ya kuanza kufanya, hali hii hutokea kwa sababu watu wengi ambao maisha yao duni huishi kwa kuogopa sana wakati ujao.

Pia akili za mwanadamu zimetawaliwa kwa kiwango kikubwa na vitu ambavyo havionekani, hapa ndipo lile somo la kujipa majibu hasi linapofanya kazi, kwa vitu ambavyo anaviwaza ambavyo kimsingi bado havijawekwa katika utekelezaji.

Kwa mfano unakuta mtu ana mawazo mengi ambayo ukiyatazama kwa "jicho la tofauti" mawazo hayo yatawezwa kubadilishwa na kuwa katika matendo yana uwezo mkubwa sana wa kubadilisha maisha ya mhusika huyo kwa asilimia mia moja, ila changamoto kubwa pindi mtu awazapo huanza kuja na vikwazo ambavyo kimsingi huwa na vitu ambavyo havimpi nguvu ya kuthubutu kutenda jambo hilo.

Hii huwa ni ishara mawazo yetu huwa ni chanya mara nyingi lakini suala zima la utekelezaji wa suala hilo huwa ni kikwazo kikubwa, lakini nikwambie neno moja ya kwamba kuanza sasa unahitaji ubongo wa ziada.

Unaweza ukajiuliza ubongo wa ziada labda ni kuwa na ubongo mwingine, la hasha sina maana hiyo ila ukweli ni kwamba uanze kufikiria katika akili nyingine ambayo itakufanya uwe mpya, katika fikra mpya hususani suala zima la kuwa na mtazamo chanya.

Inawezekana ukajiuliza unawezaje kuwa mtazamo chanya?
Suala zima kuwa mtazamo chanya huwa linatokana na kujiuliza katika mambo ambayo unayofanya, je mambo hayo yana matokeo gani katika maisha yako na watu wengine?

Watu ambao wanakuzungua huwa wanatazamo gani juu yako? Na mara zote ikumbukwe ya kwamba maisha yako yanatazamwa kwa asilimia kubwa na watu wengine, watu wanaokuzunguka wakikutazama katika jicho chanya hata kile kitu ambacho unakifanya kinaweza katika kuwa bora zaidi.

Ifike pahala jamii ambayo inakutazama wakufikirie kwamba ni mtu chanya, kufanya hivi kutakufanya uweze kujitangaza jina na kujiongezea thamani.

Amua sasa kutenga muda wa kujiuliza mambo ya msingi ambayo yatakusaidia kuwa na mtazamo chanya kwa kila jambo amabalo unakiwaza au ambalo unalitenda. Pia ikumbukwe ya kwamba ni vyema ukaamua kubadili maisha yako kwa kuwa na mtazamo sahihi.

Post a Comment

 
Top