Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamtafuta mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la Saidi Hamisi Kombo dereva wa gari yenye namba za usajili T 954
na tela lake yenye.no 397CCY aina ya Scania kwa kosa la kutoroka na
shehena ya korosho magunia 405 yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni mia moja na 22 mali ya kampuni ya Starnuts Company Limited.
Amesema dereva huyo alikabidhiwa magunia hayo ili kuyasafirisha kwenda
bandari ya Mtwara lakini mtuhumiwa huyo alitoweka mara tu baada ya
kuingia mtwara mjini.
Hata hivyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa namba za gari
alizotumia mtuhumiwa ni bandia kwani namba hizo ni za gari aina ya
Isuzu Carry na namba halisi za gari hilo ni T 852 APL na tela lake ni T
198 AKY mali ya Gulled Transport LTD inayomilikiwa na Abdi Hers wote
wakiwa wakazi wa Dar es Salaam.
Kamanda amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea na kutoa wito kwa wakazi
wa Mtwara kuwa makini na wezi na matapeli hasa kipindi hiki cha mwisho
wa mwaka ambapo vitendo vya hali hiyo vimekuwa vikiongezeka.
Post a Comment