0

wavuvi haramu
Na.Ahmad Mmow, Lindi. Kilwa Masoko.
Kufuatia msako unaondelea wilayani Kilwa wa kuwakamata wavuvi haramu wilayani humo.Wavuvi haramu 36 wamejisalimisha kwa mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai.
 
 Hayo yalielezwa juzi na mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa alipozungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini mwake, mjini Kilwa Masoko.

Ngubiagai akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, alisema kufuatia msako huo ambao aliuita vita dhidi ya watu wasio na uzalendo, umesababisha wavuvi haramu kujisalimisha kwake nakuhaidi hawatarudia kufanya uhalifu huo na watasaidiana na serikali katika mapambano hayo.

Alisema tangu kuanza msako huo, baadhi ya wavuvi haramu wamesalimisha kwa wasamaria wema zana walizokuwa wanatumia katika kufanikisha uhalifu huo.
"Wamekuja kwangu nakuhaidi hawatarejea kufanya uhalifu na watashirikiana na serikali, nawaomba wengine wafanye hivyo kabla hayajawakuta makubwa," alisema Ngubiagai.

Aliongeza kusema msako huo umefanikisha kukamatwa zana mbalimbali zinazotumika kwa uvuvi huo unaotishia kuangamiza viumbe vya baharini na makazi yao.

Mmoja wa wawavuvi haramu waliojisalimisha kwa mkuu huyo wa wilaya, Gerold Fabiani, aliyekiri kuwa alikuwa anafanya uhalifu huo kwa takribani mwaka mmoja, alisema aliamua kujisalimisha kwakuwa jina lake lilikuwa kwenye orodha ya wavuvi haramu katika wilaya hiyo.

Huku akibainisha kwamba "Orodha ya majina aliyonayo mkuu wa wilaya ni sahihi, hakuna aliyesingiziwa namimi nimiongoni mwa wavuvi haramu nakubali nikweli. Lakini kuanzia sasa nimlinzi nitasaidiana na serikali katika kuwafichua wavuvi harama," alisema na kuhaidi Fabiani.

Alisema sababu ya yeye kujiingiza kwenye uvuvi huo ni kuona wenzake walikuwa hawakamatwi na walikuwa wanapata samaki wengi kuliko yeye aliyekuwa anavua kwa njia halali. Gerold aliongeza kusema kama serikali ya wilaya hiyo itaendeleza misako hiyo na kuwamakata wavuvi haramu na wafadhili wao kunauwezekano mkubwa wa samaki kuongezeka na wao hawatakwenda umbali mrefu kuvua, kama ilivyo sasa.

Mvuvi Abdallah Ahmad, licha ya kufurahia na kuunga mkono zoezi hilo, alitoa wito kwa serikali ya wilaya hiyo kufanya misako mara kwa mara ya kushitukiza. 

Akibainisha kwamba uvuvi haramu umesababisha wavuvi wadogo kama yeye kushindwa kupata samaki. Kwa madai kuwa hana chombo cha kusafiria na kumfikisha bahari kuu. Kwasababu samaki wanapatikana mbali tofauti na miaka ya nyuma kabla ya uvuvi haramu kuanza katika wilaya hiyo.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa umoja wa wavuvi wa halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo ya wilaya ya Kilwa, Juma Mkomi, alisema licha ya serikali kufanya doria mara kwa mara lakini pia itoe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu madhara ya uvuvi haramu, kulasamaki waliouwawa kwa sumu na faida za kulinda bahari na viumbe vilivyomo baharini kwa masilahi mapana ya kizazi cha sasa nakijacho.
"Nasisi wananchi kwa upande wetu tunawajibu wa kushirikiana na serikali, tuwafichue wanaoendesha vitendo hivyo, tuunde vikundi vya ulinzi na tusaidie kutoa elimu. Maana serikali bila kusaidiwa na wananchi haiwezi kufanikiwa," alisema Juma Mkomi.

Siku hiyo zana mbalimbali zinazotumika kwa uvuvi haramu ambazo zilikamatwa kupitia msako unaoendelea viliteketezwa kwa kuchomwa moto katika eneo la Masoko Pwani.

Post a Comment

 
Top