Ndege za mashambulizi za Urusi zimetekeleza shambulio kubwa katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi mjini Aleppo.
Takribani watu 12 wameuawa na kusababisha uharibifu katika maeneo mbalimbali.
Wiki
iliyopita serikali ya Syria ilisema kuwa mashambulizi ya ndege
yatapunguzwa ili kuleta unafuu katika wiki mbili za kampeni ya anga
ambapo maelfu ya watu wamekufa na huduma za afya kuharibiwa.
Hayo yamefuata baada ya kuvunjika kwa usitishwaji wa mapigano ulioandaliwa na Urusi na Marekani.
Post a Comment