Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na hatari kubwa ya kutumbukia kwenye
machafuko, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetahadharishwa.
Mjumbe
wa UN Maman Sidikou amesema wanajeshi 18,000 wa kulinda amani wa umoja
huo ambao wamo nchini humo hawana uwezo wa kukabiliana na ghasia kama
hizo iwapo zitazuka.
Maandamano
yenye umwagikaji wa damu yamekuwa wakishuhudiwa mara kwa mara kufuatia
hatua ya kuahirishwa kwa tarehe ya uchaguzi wa rais.
Upinzani unamtuhumu Rais Joseph Kabila kwa kujaribu kukwamilia mamlaka hata baada ya kumalizika kwa muhula wake Desemba.
Watu
kadha walifariki wakati wa maandamano ya kupinga serikali mwezi jana
mjini Kinshasa baada ya tume ya uchaguzi kusema haingewezekana uchaguzi
ufanyike Novemba.
- 'Watu 50 wauawa' maandamano ya upinzani DR Congo
- Marekani yazuilia mali ya maafisa wawili wa DR Congo
Makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani yalishambuliwa na kuchomwa moto.
"Wadau
kutoka pande zote wanaonekana kuwa tayari zaidi na kutumia ghasia
kutimiza malengo yao," Bw Sidikou, mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha
UN kunachojulikana kama Monusco, aliambia baraza la usalama la UN
Jumanne.
"Ingawa Monusco itafanya kila iwezalo kulinda raia, haina uwezo wa kukabiliana na hatari zote zilizopo."Aliongeza: "Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeingia kipindi cha hatari kubwa kwa uthabiti wake. Kipindi kijacho kitakuwa kigumu sana, kuna uwezekano wa kufikia pahala ambapo ghasia zitazidi."
DR Congo haijawahi kuwa na rais aliyekabidhi madaraka kwa njia ya amani kwa mrithi wake tangu uhuru miaka 55 iliyopita.
Bw Kabila aliingia madarakani 2001 baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila.
Post a Comment