Sekondari hii ni ya serikali iliyopo ndani ya Kata ya Kiangara wilayani Liwale mkoa wa Lindi.
Akizungumza na wanafunzi,wazazi pamoja na wageni waalikwa katika mahafali ya kidato nne - 2016,Mkuu wa shule mwalimu JOSEPH KOMBA amesema kuwa,tangu kuanzishwa kwa shule hii mwaka 2007 ufaulu ulikua wa chini sana ambapo katika kila mwaka walau kwa wastani wa mwanafunzi mmojammoja tu walau walipata ufaulu wa daraja la nne hadi la tatu. Halo hii mbaya imesababishwa na jamii kutokukubali kuamka na kupokea mabadiliko ya elimu,Bali hii kwa kiasi kikubwa imechangiwa na athali za wakoloni (hasa waarabu)
Lakini kuanzia mwaka Jana (2015) kumeanza kuwa na matokeo chanya kwani ufaulu wa wanafunzi ulianza kupanda na wanafunzi watano walifaulu na kujiunga na masomo ya kidato cha tano-sita.
Kadhalika afsa mtendaji wa Kata ya Kiangara ndg. GEORGE STAMBULI aliahidi kutoa ushirikiano kudhibiti hali ya utoro shuleni hapa. Akizungumza na wazazi Stambuli alisema "Kuna baadhi ya hatua ambazo nimezichukua kwa kushirikiana na Mkuu wa shule katika kuwafuatilia wanafunzi watoro, nitoe wito kwa wazazi waachane na tabia ya kuwaficha wanafunzi huko majumbani kwani wakati huu sio rafiki,tuungane kuijenga Kiangara"
Naye Mwenyekiti wa bodi ndg. KASIMU MAKWANGU alitoa wito kwa wazazi kuendeleza umoja na mshikamano katika kustawisha taaluma hapa shuleni.
Katika hatua nyingine,mgeni rasmi katika mahafali hii ambaye ni diwani wa kata ya Kiangara Mh. HAMISI MKOPORA aliahidi kuzitatua changamoto kadhaa ainishwa katika risala. Alisema "nitahakikisha tatizo la maji,umeme, na mengineyo,nitayapeleka katika vikao vyetu madiwani na nitalisimamia na kuhakikisha yanafanikiwa" sambamba na hill aliishikuru serikali kuanzisha mafunzo ya mambo katika kata yake kwani hii ni ishara ya uwepo wa ulinzi na usalama thabiti ndani ya kata.
Katika sherehe hii,Kuna zawadi na tuzo maalumu zilitolewa kwa wanafunzi baadhi na malimu.
Baadhi ya wanafunzi waliopata tuzo maalumu ni HARUNA H.MTESA, JIANDAE MBITE, KIRUKE M. KIRUKE na AMANA P. NGULAJII.
Sambamba na wanafunzi, mwalimu NICOLAUS J. KINDOLE alipata tuzo ya uongozi bora kama mwalimu bora wa darasa na mlezi bora wa kiume (patron)
Tazama picha mbalimbali za matukio ya siku ya mahafali Jana tr. 1-10-2016.

Post a Comment