Baada ya kucheza misimu mitano kwenye klabu ya TP Mazembe, mchezaji wa
Taifa Stars, Thomas Ulimwengu ameondoka kufuata ndoto zake kucheza
Ulaya.
Mchezaji huyo aliyekuwa akivaa jezi namba 28 na aliyepewa jina la utani
‘Rambo’ alichukuliwa na klabu hiyo akiwa na umri 18 kutoka AFC Academy
ya Stockholm, Sweden. Akiwa na TP Mazembe, Ulimwengu amecheza mechi 130
na kufunga mabao 35.
Wakati anachezea klabu hiyo klabu nyingi zilitaka kumchukua lakini
aliamua kumaliza kwanza mkataba wake na Mazembe. Aliamua kutoongeza tena
mkataba na TPM. Na sasa Ulimwengu anataka kufuata nyayo za Mtanzania
mwenzake Mbwana Samatta wa Genk ya Ubelgiji.
Kabla ya kuondoka Lubumbashi, Ulimwengu alisema kupitia taarifa kwenye
tovuti ya klabu hiyo, “Kwa miaka mitano Mazembe imeniruhusu kuendelea
kukua kisoka na nataka kuwashukuru wote walioniunga mkono na kusaidia
kushinda vikombe wakiongozwa na Rais Katumbi na Mrs Carine, viongozi na
makocha.”
Post a Comment