Akina dada walioshiriki katika
mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos
jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
Mamia
walijitokeza kushuhudia maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini
Kenya. Kila siku Albino wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na viungo vyao
vya mwili kuuzwa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na
Afrika kusini.
Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada
atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa
kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza
kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi,
Kenya tarehe 21 Oktoba 2016 Wanaume
walioshiriki katika mashindano hayo wasimama jukwaani. walishiriki
katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama
Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016. Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa taji ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza.
Erick Thomas, awaongoza wanamitindo wenzake kwenye jukwaa wakati wa
mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi. Lengo lake
ni kuhakikisha kwamba watu walio na ulemavu huo wamejivunia ngozi yao. Msichana
huyu aliduwazwa na maonyesho hayo! Yeye ni miongoni mwa watu ambao kila
siku wanakabiliwa na hatari ya kuuawa kutokana na imani za kishirikina
Afrika mashariki na Afrika kusini. Miraba
minne! John Ngatia, ambaye pia huwa anasakata densi, avalia sare ya
mapigano ya ndondi katika maonyesho hayo, jijini Nairobi Kenya tarehe 21
Oktoba 2016 Majaji walikuwa macho! Waliongozwa na mwanamitindo wa kimataifa Deliah Ipupa (katikati) tarehe 21Oktoba 2016. Naomi
Wafula, ajitokeza jukwaani akiwa amevalia vazi lililotengenezwa kwa
sahani za plastiki katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini
Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016 Mamia
walihudhuria maonyesho hayo kuonyesha umoja wao na watu wanaoishi na
ulemavu wa ngozi katika mgahawa wa Carnivore jijini Nairobi Kenya,
tarehe 21, Oktoba 2016
Amina Makokha ajitokeza jukwaani akiwa
amevalia sare ya mchezo wa raga katika mashindano ya urembo
yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016 Kutoka
kulia, naibu rais wa Kenya William Ruto, Mbunge Isaack Mwaura na
mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua pia
walikuwemo.
Post a Comment