Nahodha wa timu ya
taifa ya England Wayne Rooney, amesema huu ni wakati mgumu kwake baada
ya kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza kitachocheza mchezo kuwania
kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Slovenia leo hii jumanne.
Kocha
wa muda wa kikosi hicho Gareth Southgate, amesema uamuzi wa kumuweka
benchi mchezaji huyu ni wa kiufundi na sio suala la ubora wa kiwango cha
Rooney.
Nyota huyu mwenye umri wa miaka 30, anaendelea kuwa
nahodha wa timu ya taifa lakini katika mchezo wa dhidi ya Slovenia,
Jordan Henderson, ndie atavaa kitamba cha unahodha.
Rooney, ndie mfungaji bora wa kihistoria wa England, akiwa na bao 53 akifuatiwa na sir Bobby Charlton, aliefunga bao 49.
Pia
ndie mchezaji wa pili kuichezea mechi nyingi nchi yake akiwa amecheza
mechi 117 nyuma ya kipa peter shilton aliyecheza mechi 125.
Post a Comment