Facebook imenzisha
mfumo mpya wa mtandao unaojulikana kama Workplace, ambao utaziwezesha
kampuni kubuni njia ya kufanya mawasiliano.
Mtandao huo unaofanana
na wa Facebook, na ulio na sehemu muhimu zikiwemo za kupeperusha video
moja kwa moja na kwa mawasiliano ya ujumbe, hauwezi kutumiwa na mtu
binafsi.
Mtandao huo umebuniwa kuchuchukua mahala pa mifumo mingine kama ya email kwa mawasiliano kazini.
Mdadisi mmoja alisema kuwa mtandao huo utatoa ushindani mkubwa kwa mifumo mingine washindani.
Utaingia
kwenye masoko sawa na ya mtandao wa Microsoft wa Yammer, ambao
makampuni yanaweza kutumia na ule wa Slack ambao ni wa mawasiliano ya
ujumbe.
Facebook imekuwa ikiufanyia majaribio mfumo huo ambao
awali ulifahamika kama Facebook at Work, kwa muda wa miaka miwili na
kusema kuwa hadi makampuni 1000 tayari yanautumia.
Post a Comment