Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na
wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT
Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni
rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na
kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance
Magere.
RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora, Samuel Ndebeto.
RC
Makonda akipeana mkono na mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya
Sekondari ya Jitegemee JKT, Samina Rajab baada ya kumkabidhi cheti
katika mahafali ya 32 kwa ushiriki wake wa masuala ya Skauti shuleni
hapo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
Huyu ndiye ni Mwanafunzi Bora wa Shule hiyo, Samuel Ndebeto.
Mkuu
wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali,
Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa
Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa
Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere,
Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe
wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.
Mgeni rasm Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhitimu wa kidato cha nne akisakata rhumba kwenye mahafali hayo.
Walimu na wanafunzi wakicheza kwaito.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu ndani ya ukumbi.
Mgeni rasmi Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa jukwaa kuu.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya shule hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi na walezi
kuwaacha huru watoto wao kuendelea na masomo wayapendayo badala ya
kuwachagulia.
Mwito
huo ameutoa katika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya
Sekondari Jitegemee JKT Mgulani Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni
rasmi.
"Watoto
wapewe uhuru wa kile wanachopenda kukisomea badala ya kuwachagulia kwa
kufanya hivyo itawasaidia kupenda kazi watakayoifanya kutokana na masomo
waliyosoma" alisema Makonda.
Alisema
hivi sasa kuna changamoto kubwa kwa watumishi kujiingiza katika vitendo
vya ubadhirifu kutokana na kutokuwa wazalendo kutokana na kufanya kazi
ambayo imetokana na masomo ambayo hawakuyapenda.
Alisema
kama mtoto anapenda kuwa mtaalamu wa kompyuta muache aendelee na masomo
ya kompyuta badala ya kumlazimisha kuwa na taaluma nyingine.
Mkuu
wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy alisema wahitimu hao
wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mtihani wao watakao uanza
Jumanne wiki ijayo na kuwa wanategemea wote watafanya vizuri.
Kessy
alisema kuhitimu kidato cha nne ni hatua nyingine ya kuendelea na elimu
ya juu hivyo aliwataka wahitimu hao kuondoa wasiwasi katika kipindi
hiki cha kuelekea kufanya mtihani wa mwisho.
Wakisoma
risala yao kwa mgeni rasmi Paul Makonda wanafunzi hao walisema
changaoto kubwa waliyonayo na uchakavu wa miundombinu shuleni hapo kama
mapaa ya vyumba vya madarasa kuezekwa kwa mabati aina ya Asbestors
ambayo si mazuri kiafya pamoja na uchakavu wa sakafu ambapo Makonda
aliahidi kutoa mabati 2,000 kwa ajili ya kuezekea vyumba 25.
Katika
hatua nyingine Makonda amezitaka shule za sekondari za jeshi katika
mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha zinaunda kamati kwa ajili ya kurudisha
heshima ya michezo mashuleni kama ilivyokuwa awali.
Post a Comment