SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sikika, limemwomba Rais John Magufuli
kuagiza fedha zitolewe kama mpango wa dharura kutatua tatizo lililopo la
dawa nchini ikiwa ni pamoja na kulipa deni lote la Bohari Kuu ya Dawa
(MSD).
Aidha, limependekeza Bohari Kuu ya Dawa iachwe iwe taasisi au kampuni huru itakayofanya maamuzi yake yenyewe na kukusanya mtaji kushindana na wauzaji wengine binafsi wa dawa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irene Kiria, alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni, Dar es Salaam na kueleza kwamba mojawapo ya sababu za uhaba wa dawa ni serikali kushindwa kutenga fedha na kutoa fedha za kutosha kukidhi mahitaji ya nchi na dawa muhimu na vifaa vya tiba.
“Kwa mfano, mahitaji ya sasa ya dawa na vifaa tiba ni zaidi ya Sh bilioni 577, lakini bajeti iliyotengwa kwa mwaka huu ni Sh bilioni 251, ambapo kati ya hizo, Sh bilioni 108 ni za kulipa deni la MSD,” alieleza Kiria na kusisitiza kuwa licha ya tamko la serikali wiki iliyopita, ni ukweli kuwa kuna uhaba wa dawa kwa asilimia 47.
Kiria alisema kutokana na uzoefu wa Sikika wa kufanya kazi na sekta ya afya kwa takribani miaka 10, imependekeza serikali ifute ulazima wa vituo vya kutolea huduma za afya vya umma kuagiza dawa MSD kwanza, badala yake viachwe huru kuamua kununua kutoka kwa muuzaji yeyote mwenye dawa ambaye anadhibitiwa na kuhakikiwa na serikali.
Pia aliwaomba watendaji na viongozi katika sekta ya afya wafanye kazi kitaalamu zaidi badala ya kisiasa, huku akieleza kuwa uhaba wa dawa na vifaa tiba MSD siyo tatizo jipya, bali ni la muda mrefu na serikali imekuwa ikikiri isipokuwa sasa limekuwa kubwa hata kusababisha uhaba wa dawa kama za chanjo kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu.

Post a Comment