0

Ipo faida kubwa maishani mwako endapo utaamua leo kuchukua hatua mathubuti ya kutaka kufanikiwa. Tupo hivi tulivyo kwa sababu hututaki kuchua hatua sitahiki za kiutendaji kwa yale yalipo akilini mwetu na kuyaweka katika matendo. Watu wana maarifa lakini suala la kuyaweka maarifa hayo katika matendo.

Kuwepo kwa hali hii ndiyo ambayo inasababisha kuweza kuyatamani mafanikio na si kuyaishi. Hata hivyo moja ya siri nzito ya mafanikio yako husukumwa na kiu kubwa sana aliyonayo mtu  kutaka kufanikiwa, lakini kiu hiyohiyo huendana na msukumo na nia thabiti ya kuyaweka yale unayoyajua katika matendo.

Nasisitiza hili kwa sababu moja kubwa watu wengi wanaishi maisha ya kawaida kwa sababu wameamua hali hiyo kutokea, lakini ili kuondokana na hali hii huna budi leo hii kuacha kuishi kikawaida kwa sababu wewe sio mtu wa kawaida.

Huenda ukawa unajiona wewe ni mnyonge katika maisha kwa sababu labda uliwahi kufeli kwenye jambo fulani ambalo ulitegemea ya kwamba litakupa matokeo chanya lakini matokeo yake yakawa kinyume chake. Lakini Amini usiamini ila ukweli ni kwamba watu wengi ambao wamefanikiwa wao walikuwa ni watu ambao hawakutaka kuishi kikawaida.

Hivyo hajalishi umefeli kwa kiwango gani ila lakini iambie nafsi yako ya kwamba wewe si mtu wa kukata tamaa bali ni mtu wa kusonga mbele kivitendo zaidi.

Kuishi kikawaida ni sumu sana katika maisha yako. Wapo baadhi ya watu wamefeli kimaisha kwa sababu walikatishwa tamaa na watu wengine, huenda ukawa ni wewe ambaye unasoma makala haya ila ukweli ni kwamba maisha halisi ya kwako unayo wewe na si mtu mwingine haijalishi watasema nini ? Ila we songa mbele kivitendo ila pale unapofanikiwa wabaki midomo wazi.  Maana dunia hii imejaa wakatishaji tamaa.

Na kila mara tuzidi kuukumbuka ule usemi mtamu ambao unasema usiwambie watu ndoto yako, bali waosheshe ndoto hiyo kwa vitendo zaidi. Kwani kuwashirikisha watu juu ya ndoto yako, wapo baadhi ya watu endapo utawaambia jambo lako asilimia kubwa watakwambia haiwezekani.

Pia kwa kuwa maneno yana nguvu sana utajikuta kweli umeshindwa kuifanya hiyo ndoto yako . Simama imara kila mara kwa sababu wewe ni mshindi katika ulimwengu huu.

Kabla sijaweka nukta siku ya leo, nikandamizie maneno haya ya kwamba ili uweze kushinda vita vya umaskini, hautitaji uongozi imara kama ambavyo tumekalilishwa mashuleni, ila unahitaji kuwa bora kwa jambo lolote unalolifanya.

Kama ni biashara hakikisha unazalisha bidhaa yenye ubora kila mara, ukifanya hivi ni chachu kubwa sana ambayo itafanya wateja waongezeke wenyewe na si kuwa na kiongozi bora katika eneo lako unaloishi.

Nasema masuala haya ya uongozi  kwa sababu idadi kubwa wanahusisha masuala ya maisha yao kuwa magumu na masuala mazima ya uongozi, lakini ukweli ni kwamba ukifanya uchunguzi wa kutosha juu ya maisha yako utagundua ni nini ambacho nasema.

Maisha yako kuwa magumu usiyahusishe na masuala ya uongozi, bali tafakari katika kila kona ambayo unafanya kazi kwa kufikiri ni namna gani unaweza kuwa bora? Ukipata majawabu sahihi ya jinsi ya wewe kuwa bora hiyo siri kubwa ambayo ipo kwako ya wewe kufanikiwa.

Kama ni mwanafunzi fikiri jinsi ambavyo utakuwa bora katika taaluma yako, kama wewe ni msanii katika eneo lolote lile fikiri ambavyo utaweza kufanikiwa na sio kushirikisha imani potofu kutofanikiwa kwako na imani ambazo sio za msingi.

Dunia ni pana ila kwa maneno machache sana, kwa leo niishie hapo tukutane mara nyingine ambapo tutazidi kuelimishana masuala mazima ya mafanikio. Hivyo nikunong'oneze badili mfumo wa maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi.

Post a Comment

 
Top