Facebook imezindua aina mpya ya programu tumishi yake ya kutuma ujumbe ambayo inawalenga watu wa mataifa yanayoendelea.
Programu
hiyo mpya ya Messenger, ambayo inaitwa Messenger Lite, itaanza kutumiwa
nchini Kenya, Tunisia, Malaysia, Sri Lanka na Venezuela kwanza.
Itazinduliwa katika nchi nyingine baadaye.
Messenger
Lite imeundwa kutotumia sana data, jambo ambalo huwa tatizo kubwa
mataifa yanayoendelea kutokana na gharama pamoja na kasi ya mtandao.
Programu hiyo ya simu za Android pia inaweza kufanya kazi kwa urahisi maeneo ambayo huduma ya mtandao si ya kutegemewa.
"Messenger
Lite ukubwa wake ni chini ya 10MB, hivyo ni rahisi sana kuiweka kwenye
simu na kuifungulia," taarifa ya Facebook imesema.
"Inatumia nembo inayokaribiana na ya Messenger, lakini rangi zake ni kinyume."
- Satelaiti ya kufikisha mtandao kasi Afrika yaharibiwa
- Mark Zuckerberg ala ugali Kenya
- Video ya mwanamke akijifungua kwenye maji
Wanaotumia programu hiyo ya Messenger Lite kwenye simu zao bado
wataweza kutumia huduma muhimu zikiwemo uwezo wa kutuma ujumbe, picha na
vihusishi vya kurasa za mtandao.
Hata hivyo, hawataweza kupiga
simu za kawaida au za video kwa kutumia programu hiyo kama ilivyo kwa
programu za kawaida za Messenger.
Facebook pia huwa na aina
'nyepesi' ya programu tumishi ya Facebook ambayo huitwa Free Basics na
ambayo hufaa sana watu wasio na huduma ya kutegemewa ya mtandao.
Programu hiyo hupatikana katika mataifa kadha.
Afisa
mkuu mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg mara kwa mara amekuwa akisema
lengo ya kampuni yake ni kuhakikisha kila mtu duniani anaweza kutumia
huduma ya mtandao.
Inakadiriwa kwamba watu bilioni moja duniani hutumia programu ya Messenger kutuma au kupokea ujumbe kila mwezi.
Post a Comment