0
Mgeni rasmi wa mahafali ya shule ya Sekondari Makata,Bw. Hasani Mpako akizungumza na wazazi,walezi na walioudhulia kwenye mahafali jana octoba 13. 

MAHAFARI YA KIDATO CHA NNE,LIWALE-LINDI
Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Makata,John Malima akisoma risala kwa niaba ya shule hiyo kwa wanafunzi,wazazi,walezi pamoja na wageni waalikwa katika mahafali ya kidato nne -2016,amesema kuwa shule hiyo inachangamoto mbalimbali akiwemo wanafunzi kutembea umbali wa kilometa 8 kufuata masomo shule hapo kwa ukosefu wa mabweni.

Mwalimu mkuu alisema moja ya changamoto kubwa ukosefu wa mabweni alibainisha katika wahitimu hao walianza wakiwa jumla ya wanafunzi 51 na mpaka sasa wanahitimu wakiwa wanafunzi 25 kati yao wavulana 17 na wasichana 8 na jumla ya wanafunzi wote katika shule ni 168 na inajumla ya madarasa 8.

Changamoto zingine ni ukosefu wa walimu wa sayansi,upungufu wa choo,ukosefu wa nishati ya umeme na upungufu wa nyumba za walimu ikiwa shule hiyo ina jumla ya walimu 12,wanaume 10 na wanawake 2 na nyumba za walimu shuleni hapo zipo 2 na kulazimika walimu kulala wawili wawili.
 Katika hatua nyingine,mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha umoja (UMOJA AMCOS) Bw.HASANI MPAKO aliahidi kuzitatua changamoto kadhaa ainisha katika hutuba yake.Alisema "chama cha umoja amcos moja ya malengo yake ni kusaidia jamii hiyo tutatoa msaada wa magodolo 50 ikiwa moja ya kuhakikisha watoto wetu wanakaa bweni na kupata elimu bora"

Pia katika hatua ingine ya kusaidia kutatua changamoto mgeni rasmi,Mpako atatoa mifuko ya saluji 20 kwa ujenzi wa choo na alitoa shilingi laki moja kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi siku ya kufanya mtihani.

Mpaka aliwaomba wazazi na walezi pamoja na wadau wengine kuunga mkono katika kutatua baadhi ya changamoto kwa kuchangia mbao au fedha kwa ajili ya utengenezaji wa vitanda vya wananafuzi katika shule hiyo na asisitiza mahusiano mazuri kati ya walimu na viongozi wa wilaya.

Diwani wa kata hiyo ya Makata,Mhe.MFAUME MPUNGU alisema ataendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali katika kuhakikisha kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba shule hiyo.
Wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Makata iliyopo katika Kata ya Mataka wilayani Liwale mkoa wa Lindi.

 Angalia  picha mbalimbali za matukio ya siku ya mahafali yaliyofanyika  octoba 13 2016.

 
Hassani Ally Ngaomela akisoma risara 
                                Mwanafunzi akikabidhi risara kwa mgeni rasmi

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Makata,John Malima akisoma risara na kuwaeleza wazazi na walezi baadhi ya changamoto za shule hiyo
 Mgeni rasmi akizungumza na wahitimu,wazazi,walezi na wadau mbalimbali walioudhulia kwenye mahafari yaliyofanyika katika shule ya sekondari Makata octoba 13, 2016
Mgeni rasmi Bw. Hasani Mpako akitatua moja ya changamoto hapo hapo ikikabidhi shilingi laki moja
Mwenyekiti wa bodi ya shule akipokea shilingi laki moja kutoka kwa mgeni rasmi
 wahitimu wa kidato cha nne wakisiliza kwa umakini hutuba ya mgeni rasmi huku waelezwa wakitaka kutimiza ndoto zao alazima wawe na mambo manne ikiwa ni kuwa waminifu,wavumilivu,kujituma na kutokata tamaa
 wanafunzi wa shule wa sekondari walioudhulia katika mahafari ya kuwahaga kaka na dada zao
 wazazi,walezi pamoja na wadau mbalimbali walioudhulia kwenye mahafari hayo octoba 14 mwaka 2016


Diwani wa kata ya Makata,mhe. Mfaume Mpungu akiambapata na diwani wa viti maalum aliyekaa upande wa kulia
Hatua ya ugawaji wa zawadi mabalimbali ikiwa vyeti maalum kwa wahitimu zilianza
 Mgeni rasmi Bw.Hasani Mpako akiongoza zoezi la kukabidhi vyeti maalum na vyeti vya uthibisho kwa wahitimu wa kidato cha nne









Post a Comment

 
Top