Mwanza. Wakati Serikali ikikosa mapato ya zaidi ya Sh1 trilioni
zitokanazo na kodi ya makazi, wananchi hupoteza mtaji wa Sh6 trilioni
kwa kuishi kwenye nyumba zisizo na hatimiliki.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema hayo kwenye kikao na watendaji na madiwani wa halmashauri za Jiji la Mwanza na Ilemela alikofanya ziara ya siku moja na kukabidhi hati zaidi ya 10 za makazi.
Kutokana na kodi na mtaji kupotea, Lukuvi ameuagiza uongozi wa Serikali mkoani Mwanza kuhakikisha halmashauri zinakamilisha kazi ya kurasimisha makazi holela ifikapo Juni 30, mwakani ili kuongeza ukusanyaji wa mapato na upatikanaji wa mitaji kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema Januari Mosi mwakani watakamilisha kazi hiyo kwa kuwa kuna wataalamu 98 kwenye Jiji la Mwanza na Ilemela watakaosaidiana na wenyeviti wa mitaa kufanya kazi ya kurasimisha makazi.
Lukuvi amesema utafiti umebaini makazi zaidi ya 35,000 jijini Mwanza yamejengwa maeneo yasiyo rasmi.
Amesema wizara ina upungufu wa wataalamu wa kupima viwanja, hivyo itawatumia wa binafsi kutoka kampuni 58 kupanga maeneo ya makazi.
Mkazi wa Buhongwa, Sophia Mashishanga (70) ni miongoni mwa waliokabidhiwa hati na Lukuvi alimpongeza kwa uvumilivu wa kusubiri hati hiyo.
Robert Joseph, alisema ni jambo la kihistoria kupata hati ambayo ameifuatilia kwa miaka 30.
Wakati huohuo, Lukuvi alisema wizara imeshusha kodi ya hati ya makazi kutoka Sh160,000 hadi Sh50,000, huku ikipunguza asilimia ya tozo ya kodi kutoka saba hadi 2.5. Pia, amefuta kodi zinazotozwa kwenye nyumba na taasisi za umma kama vile shule na hospitali, akiagiza wenyeviti wa mitaa kuyapima maeneo hayo na yatalipiwa Sh 5,000 kwa mwaka.

Post a Comment