Baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara mkoani Arusha
wameshindwa kuendelea na kazi kutokana na ukosefu wa maji
kulikosababishwa na kukauka kwa vyanzo vya maji.
Wakiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi kwenye kikao cha bodi ya
barabara mkoa wahandisi wa wilaya zinazokabiliwa na tatizo hilo ikiwemo
ya Ngorongoro wamesema tatizo hilo ni kubwa na kazi zote zinazohitaji
maji katika miradi hiyo zimesimama hadi hapo mvua zitakaponyesha kwani
kiasi cha maji kinachopatikana hakiwezi kukidhi mahitaji.
Katika hatua nyingine mhandisi wa mkoa bw,edwaerd amboka amesema pia
katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya barabara wamebaini kuwepo
kwa wakandarasi wamebainika kuwepo kwa baadhi ya wakandarasi wasio na
uwezo na waliopata tenda kwa udanganyifu na huku Katibu Tawala
anayeshughulikia miundombinu naye akielezea uwepo wa tatizo la matumizi
mabaya ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya miundombinu.
Akizungumzia tatizo la kusua sua kwa miradi na mingine kusimama kutokana
na tatizo la maji mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkuu wa mkoa
wa Arusha Bw Mrisho Gambo amesema zipo taratibu za kufuata
zinazpojitokeza changamoto kama hizo na kuhusu wakandarasi
walioidanganya serikali ameviagiza vyombo vinavyohusika ikiwemo TAKUKURU
kuhakikisha sheria inachukua nafasi yake kwa wote walioshiriki
kufanikisha udanganyifu huo.
Arusha ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na tishio kubwa la ukame
linalohusishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi,ukame na uharibifu wa
mazingira ambao umesababisha asilimia kubwa ya vyanzo vya maji
kukauka,na kwa sasa asilimia kubwa ya wananchi wanategemea maji visima
ambavyo hata hivyo bado ni upatikanaji wake ni mgumu.
Post a Comment