Kama
umekuwa karibu na mitandao mbali mbali basi lazima utakua hukupitwa na
ile habari ya kijana kutobolewa macho huko Buguruni Dar Es Salaam. Sasa
hapa ni taarifa za majibu ya madaktari juu ya uchunguzi wa Macho ya
kijana Said maaarufu kama Baba D ambaye alipata mkasa wa kushambuliwa na
mtu anayefahamika kwa jina la Scorpion, kisha kutobolewa macho yote
mawili hali iliyopelekea kutoona.
Jitihada
zilizofanywa na Serikali ya mkoa wa Dar es salaam zikiongozwa na mkuu
wa mkoa Paul Makonda ili kuweza kumsaidia kijana huyo zilifanikiwa
kumfikisha katika Hospitali ya Muhimbili ambako alifanyiwa uchunguzi wa
kina ili kujua kama kuna uwezekano wowote wa kumrejeshea uwezo wa kuona.
Post a Comment