0

Chama cha Wananchi (CUF), kimeendelea kudai kuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad alishinda na kunyang’anywa ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Akizungumza mjini hapa jana, Maalim Seif ambaye pia ni katibu mkuu wa chama hicho, amesema hakuna namna yoyote watawala wataweza kuzuia haki ya uamuzi wa Wazanzibari walioutoa Oktoba 25, 2015, lakini kinachoendelea ni njama za kuichelewesha.

Maalim amesema hayo wakati akitoa salamu kwa waumini wa Dini ya Kiislamu waliofika kwenye ibada ya Ijumaa katika Msikiti wa Biziredi.

CUF wanalalamikia ushindi huo zikiwa zimepita siku 215 tangu uchaguzi wa marudio ulipofanyika Zanzibar.

Post a Comment

 
Top