0

                                     Mchezaji wa timu ya ABC fc akirusha mpira
                      Mchezaji wa timu ya Black Stars akimiliki mpira uwanjani


Mchezo wa leo octoba 26 kati ya timu ya Black Stars dhidi ya ABC (Mpengele)fc umemalizika kwa sare ya magoli 2 kwa 2 mchezo uliochezwa uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Black stars ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu namo dakika ya 9 lililofungwa na Hamisi Lipikwe na goli la poli lilifungwa na Kasimu Ngalondola dakika ya 43.

Magoli ya timu ya ABC fc yalifungwa na Ali Mapui katika dakika ya 12 na goli la pili likifungwa na Sharifu Mahaku dakika ya 27.

Kocha wa timu ya ABC fc,Twaibu Matengana akiongea na mwandishi wetu alisema mchezo wa leo ulikuwa mzuri pia waliweza kuumiliki mchezo katika kipindi mara baada ya mlinda lango wao Chande Mmiche kuumia na kupoteza fahamu na kulazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya kumaliza hisabu.

Kwa upande wa kocha wa timu ya Black Stars,Maulidi Mpalama alisema mchezo ulikuwa mzuri na hali ya waamuzi wameweza kuzesha vizuri na aliongeza kusema mchezo ujao anatarajia kupata pointi 3.

Siku ya kesho alhamisi octoba 27 kutakuwa na mapambano wa watani wa jadi watakaoshuka dimbani kati ya timu ya Sido fc dhidi New generation,timu ya New generation tayari imeanza kupata pointi 3 tayari baada ya kuilaza timu ya Nangando fc mabao 3-0 octoba 24 huku timu ya sido fc ikiwa ndio mchezo wao wa kwanza.

Post a Comment

 
Top