Watu
kumi wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa kutokana na ajali ya
Basi la kampuni ya Barcelona iliyo tokea jana katika kijiji cha Miteja
wilaya ya Kilwa, mkoa wa Lindi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii kutoka wilayani Kilwa, mkuu wa wilaya hiyo,
Christopher Ngubiagai, amesema ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha
Miteja, baada ya gari ya abiria ya kampuni ya Barcelona iliyokuwa
inatoka jijini Dar-es-Salaam kwenda Tandahimba mkoa wa Mtwara, kupinduka baada ya kupasuka gurudumu la mbele.
Ngubiagai
ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo
amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 10 na wengine 44
kujeruhiwa.
"Ajali
imetokea leo(Jana) saa nne asubuhi, changamoto iliyopo hapa nikwamba
chumba cha kuhifadhia maiti hakina majokofu ya kutosha kuhifadhia maiti
kumi, tunaangalia uwezekano wa kusafirisha miili hiyo hosipitali ya
mkoa," alisema Ngubiagai.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kuangalia usalama na uhai wa abiria badala ya faida pekee.
Akibainisha kuwa pamoja na mwendo wa kasi, lakini pia ajali hiyo imechangiwa na uchakavu wa magurudumu.
"Tairi(magurudumu)
za gari ile ni vipara kabisa, hata kondakta analalamika nakusema mara
kadhaa walimshauri mmiliki anunue tairi mpya lakini hakuwasikiliza," alisema Ngubiagai.
Pia
mkuu huyo wawilaya amelaumu umakini wa askari wa usalama barabarani kwa
kuruhusu gari hiyo iendelee na safari kutoka Dar-es-Salaam hadi eneo
iliyopata ajali wakati waliona magurudumu yake yalikuwa hayafai.
Kwa
upande wake, kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, kamishna msaidizi
mwandamizi wa polisi, Renatha Mzinga. Amethibitisha kutokea ajali hiyo,
nakuzitaja namba za usajili za gari hiyo aina ya Yu Tong, kuwa ni T110CCU.
Ambae nae alisema "Licha ya kutembea kwa mwendo mkali,lakini lakini
ilizidisha abiria, kwasababu uwezo wake ni kubeba watu 48. Hatahivyo
ilibainika kwamba ilipakia watu 54.
Kamanda Mzinga alisema kati ya majeruhi hao, watano wana hali mbaya.
"Majeruhi wa nne wanatibiwa katika hospitali ya Tingi,ambapo arobaini wanatibiwa katika hospitali ya wilaya ya Kilwa" alisema kamanda Mzinga.
Huku
akibainisha kwamba dereva wa gari hiyo bado hajapatikana na hata jina
lake halijapatika. Ambapo kondakta wake ambae pia jina lake
hajatambulika, anaendelea kupata matibabu katika hosipitali ya wilaya.
Post a Comment