0
Baada ya kubanwa na Ndanda FC kwa kulazimishwa suluhu mkoani Mtwara, Yanga imejipoza kwa Majimaji kwa kuichapa magoli 3-0 kwenye mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

Yanga iliandika bao la kwanza dakika ya 35 kipundi cha kwanza likifungwa na Deus Kaseke akiunganisha mpira wa mkwaju wa penati ya Msuva uliogonga mwamba.

Amis Tambwe amefunga magoli mawili, Tambwe alifunga bao la kwanza lake la kwanza dakika ya 75 baada ya golikipa wa Majimaji kupangua krosi ya Msuva kisha Mrundi huyo akausukumia kambani kwa kichwa. Dakika 10 baadae Tambwe alipachika bao lake la pili akiitendea haki krosi ya Juma Mahadh.

Kaseke kafunga goli lake la pili kwenye ligi baada ya kucheza mechi tatu. Alifunga goli la kwanza kwenye mechi dhidi ya African Lyon.

Tambwe amefunga magoli mawili kwenye mechi moja baada ya kucheza mechi mbili za kwanza za VPL bila kufunga goli.

Yanga imefunga magoli matatu kwenye mechi moja kwa mara ya pili, walifanya hivyo kwenye mechi dhidi ya African Lyon.

Yanga imefunga jumla ya magoli 6 hadi sasa baada ya kucheza mechi 3 huku ikiwa haijaruhusu goli.
Majimaji imepoteza mechi zote nne ambazo imecheza hadi sasa.

Matokeo ya mechi nyingine
  • Mbeya City 1-2 Azam
  • Ruvu Shooting 1-0 JKT Ruvu
  • Mwadui FC 2-2 Stand Unied
  • Ndanda FC 0-0 Kagera Sugar

Post a Comment

 
Top