0

Wakala wa Usajili wa leseni na biashara (BRELA) imewakata wafanyabiashara na wajasiriamali nchini kutumia fursa ya uwepo wa wakala hao katika kurasimisha biashara zao ili serikali iwatambue na kutoa ushirikiano katika kufanya biashara.

Msajili Mkuu waBbrela Bwana. Frank Kanyusi ameyasema hayo wakati wa zoezi la usajili wa majina ya biashara na makampuni la papo kwa papo lililoendelea mkoani hapa na kueleza kuwa lengo ni kutengeneza mazingira mazuri ya ufanyaji biashara.

Bw.Kanyusi amesema zoezi hilo ni endelevu kwa nchini nzima katika kuhamasisha wananchi kurasimisha biashara zao ili wapate urahisi wa kufanya biashara pia amesema mwitikio wa watu katika kusajili ni mkubwa kwani wameweza kusajili majina ya biashara 150 na makampuni 100 kwa siku sita.

Mmoja wa wafanyabiashara mkoani Mwanza Bwana.Andrew John amesema ni faraja kwake kwa BRELA kufika Mwanza kwani wamepata elimu juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara pia aliomba wakala hawa kufungua ofisi za kanda ili kutoa huduma kwa ufanishi zaidi.

BRELA inaendesha zoezi la kutoa elimu juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara katika kanda ya ziwa kwa kuanza na mkoa wa Mwanza na kuwataka wafanyabiahsra na wananchi kwa ujumla katika mkoa wa Mara na Geita kuwa tayari kwa zoezi hilo wiki ijayo.

Post a Comment

 
Top