aliwasili mkoani humo katika ziara yake ya kikazi kugagua shughuli za maendeleo zinazohusu wizara yake. Miongoni mwa maelekezo aliyoyatoa kwa uongozi wa TRA ni kuhakikisha wafanyakazi wanne wa mamlaka hiyo wanaofanya kazi katika kituo hicho kidogo Forodha cha Manyovu, kilichopo mkoani Kigoma wanaondolewa baada ya kubainika kuwa wanafanya kazi chini ya kiwango na kubainishwa na wafanyabiashara mkoani humo kwamba wanajihusisha na vitendo vya rushwa.
Aidha mmoja kati ya wafanyabiashara hao alisema, “Gari likifika pale Manyovu nyuma ya gari ambapo mwishoni mwa mzigo kunawekwa magunia ya mkaa kwa wafanyabiashara wale, wakifka pale mpakani mzigo unashuka ule mkaa unakuwa hongo kwa watumishi wa TRA na olisi na migration waliopo pale mpakani.”
Kwa upande wake Dk Mpango alisema, “Watumishi wengine hawakusanyi mapato na mengine mmeyasikia leo, waondoe pale, waambie Kidati waambie waziri ameyachoka, wako watanzania wenye uchungu wa nchi yao hatuwezi kuendelea kuangalia watu ambao wanaruhusu magendo yanapita na wao they are part of it”,alisisitiza.
Pia aliwaasa wafanya kazi wa taasisi hiyo kufanya kazi zao kwa uadilifu na kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya serikali na kwamba hawatamuonea huruma mfanyakazi yeyote atakayejihusisa na wizi wa fedha za umma.
“Lazima tuijenge TRA mpya ili wananchi waone kumbe ni chombo chao cha kuwaongezea uwezo wa kuwaletea maendeleo,”alimalizia