0
Mwanafunzi  wa kidato cha nne alimteka nyara mtoto wa miaka mitatu baada ya kumpa dawa za kulevya.

Mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya upili ya Maralal kaunti ya Samburu alisemekana kumteka nyara mtoto wa miaka mitatu baada ya kumpa madawa ya kulevya.

Mwanafunzi huyo alienda mafichoni na mtoto huyo, huku akimtaka mamake mtoto  kutoa  Ksh 170,000 huku akidai kumuua mtoto huyo iwapo hangepewa pesa hizo.

Joy Lekimain, mamake mtoto alihofia maisha ya mwanawe, jambo lililomfanya kutuma Ksh 2,500.

“Inaonekana alimpa mtoto dawa za kulevya kabla ya kuenda mafichoni katika kaunti ya Nyahururu,umbali wa kilomita 226 kutoka Maralal. Alipiga simu akitishia kwamba atamdhuru mtoto iwapo hatapewa fidia ya Ksh 170,000 kwa muda wa siku tano,” alisema kamanda wa polisi kaunti ya Samburu,Francis Kumut.

Hata hivyo ilisemekana kuwa mtekaji nyara huyo alikuwa wa jamii moja na mtoto huyo .

Alipatikana siku sita baadae akiwa amejificha kwenye nyumba moja katika mtaa wa Chang’aa kaunti ya Nyahururu.

Post a Comment

 
Top