Ukosefu wa usawa
"umekithiri " katika in Hollywood, huku wanawake, jamii za walio
wachache, wapenzi wa jinsia moja pamoja na wenye jinsia ya kike na ya
kiume wakiwa miongoni mwa watu wanaotengwa, utafiti mpya umebaini.
Repoti
ya chuo kikuu cha Southern California inaonyesha kuwa ni wanawake hadi
asilimia 31.4% tu waliokuwa na nafasi za kuzungumza katika filamu 100
maarufu za mwaka 2015, ikilinganishwa na 32.8% za mwaka 2008.
Wachezaji
filamu ambao ni wapenzi wa jinsia moja wa kike, wapenzi wa jinsia moja
wa kiume ama wenye jinsia zote mbili walikuwa ni chini ya 1% ya wale
waliozungumza kwenye filamu - ama or 32 kati ya wachezaji filamu
35,205.
Watafiti waliielezea Hollywood kama "kitovu cha utamaduni wa ukosefu wa usawa''.
Hata hivyo walisema kuna mafanikio madogo katika kuwahusisha watu wa tabaka mbali mbali katika Hollywood.
Baina
ya mwaka 2007, wakati uchunguzi ulifanyika kwa mara ya kwanza, na mwaka
2015, watafiti walisema kuwa hakukuwa na ishara zozote za mabadiliko ya
usawa katika uwiano wa ushirikishi wa wachezaji filamu kutoka jamii za
weusi, walatino na waasia - kiwango kikiwa 12.2% weusi, 5.3% walatino
na 3.9% waasia
Mkuu wa utafiti huo Stacy Smith, profesa katika USC, anasema: "tunashuhudia ukosefu wa usawa uliokithiri.
"iwe
tunapoangazia jinsia, jamii, rangi na hata wachezaji filamu wenye
ulemavu, kwa kweli tunaona msukumo wa kuwatenga watu wote ambao si
wazungu.
"licha ya kanuni na juhudi za wanaharakati na taarifa
zote za habari, ni mwaka mwingine ambapo tunashuhudia hali ikiendelea
kuwa ile ile bila mabadiliko yoyote.
Post a Comment