0

Serikali imesema imejizatiti katika kuwandaa wataalam wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na masuala ya usalama wa mitandao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Faustine Kamuzora kwenye mkutano uliowakutanisha wataalam wa masuala ya mtandao kutoka Tanzania na nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola, unaojadili njia za kuzuia uhalifu mtandaoni na watu kulinda matumizi ya mtandao.

Amesema usalama kwenye mitandao ni jambo la muhimu kwa vile hasara zinazosababishwa na kukosekana kwa ulinzi kwenye mtandao ni kubwa duniani kote, na kwa mwaka jana Dola Bilioni 400 zimepotea kutokana na uhalifu wa mitandaoni .

Kwa upande wake, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Joshua Mwangasa ambaye ni Afisa Kitengo cha Mitandao cha Jeshi la Polisi amesema mafunzo hayo ya usalama mitandaoni yatavisaidia vyombo vya usalama kupunguza uhalifu huo.

Post a Comment

 
Top