0


Mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,mhe. Sarah Chiwamba akizungumza na wananchi mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi wa mazingira.

Wananchi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi wamesema sheria ya usafishaji wa mashamba ya mikorosho utakuwa mgumu utekelezaji wake kwakuwa serikali ndio kikwanzo  namba moja kutokana na bei ya korosho yaubabaishaji pamoja na soko lake si la uhakika ukilinganisha na uendeshaji wake.


Changamoto hizo za wananchi zilitolewa septemba 24 kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe. Sarah Chiwamba aliopozungumza na wananchi  mara baada ya kukamilika zoezi la usafi wa mazingira katika soko kuu la Liwale.
 Katika kwenye mkutano huo mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale,Rustick Mtama aliweza kuwakumbusha wananchi sheria ndogo za usafi wa mazingira pamoja na sheria ya usafi wa mashamba ya mikorosho agizo lilotolewa na mkuu wa mkoa wa Lindi,mhe. Godfrey Zambi.

wananchi hao walibainisha sababu zinazopelekea wakulima kuacha kuyafanyia kazi mashamba ya mikorosho kutoka na bei ya kuuzia ni ya ubabaishaji na wakulima wanatumia gharama kubwa ya uendeshaji kama serikali itawajali wakulima hao hakuna mashamba yatakayoachwa bila kupaliliwa.

Mkuu wa wilaya mhe, Chiwamba awata wakulima kuacha tabia ya  kuuza mashamba yao kwa shida ndogo ndogo za muda mfupi pia amewata wakulima kuyatunza mashamba yao kwa faida ya familia zao.

Post a Comment

 
Top