0

File Photo 
Mwanza. Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepata hasara ya zaidi ya Sh125 milioni kutokana na walimu wakuu na wakuu wa shule 62 za msingi na sekondari kusajili majina hewa ya wanafunzi.

Mkurugenzi wa jiji hilo, Kiomoni Kibamba amesema hasara hiyo inatokana na walimu 37 wa shule za msingi na 25 wa sekondari kuidanganya Serikali kwamba wameandikisha wanafunzi 8,017.

Hata hivyo, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Nyamagana, Asha Juma amesema hana taarifa za suala hilo na kwamba watazifuatilia tuhuma zinazowakabili walimu hao.

Awali, Kibamba alisema walimu hao wamesimamishwa kazi kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu, ikiwamo kuwafikisha kwenye Tume ya Maadili ili wajieleze.

Post a Comment

 
Top