VIJANA 7,170
waliojiunga kwa kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
wameajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama kuanzia mwaka 2010 mpaka
sasa.
Waziri wa
Ulinzi na JKT, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema, kuanzia mwaka huo JKT
huchukua vijana 5,000 hadi 7,000 kwa madhumuni ya kuwapa stadi za kazi
na kuwajengea uzalendo.
Akizungumza
katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya Shirika
la Utangazaji Taifa (TBC1), Dk Mwinyi alisema kuanzia mwaka 2010 vyombo
vya ulinzi na usalama viliacha kuajiri kutoka uraiani, bali vijana
waliopitia mafunzo hayo ambapo zaidi ya vijana 2,000 wamekuwa
wakiajiriwa kwa mwaka.
Alisema pia
kwa sasa kuna taasisi nyingi zimeanza kuchukua vijana waliopitia mafunzo
hayo kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Hifadhi za
Taifa (Tanapa) na kampuni binafsi za ulinzi.
Habari : THEOPISTA NSANZUGWANKO
Chanzo : Habari Leo
Post a Comment