Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
Dar es Salaam. Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi,
imepokea kiasi cha Shilingi 6.3bilioni kutoka kwa Shirika la Misaada
na maendeleo la Uingereza (DFID) kwa ajili ya kufanyia ukarabati wa
shule zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Waziri wa Elimu na mafunzo
ya ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema msaada huo utasaidia kujenga
shule za Ihungo na Nyakato ambazo zimeharibika kwa kiasi kikubwa.
"Shule hizo zitajengwa vizuri na kwa uimara zaidi ili kuzuia matatizo ya aina hiyo pindi yatapo tokea tena" amesema.
Amesema fedha hizo zimetolewa na shirika hilo mara moja hivyo ujenzi na
ukarabati utaanza mara moja ili kuondoa adha wanayoipata wanafunzi.
"Utaratibu umeshafanyika na wakandarasi wanaendelea na taratibu ili kuanza ujenzi huo" amesema
Post a Comment