Mhandisi wa Mkongo wa Taifa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),
Nsaji Mwamukonda (kushoto) akizungumza na mmoja wa wakandarasi kwenye
banda la maonesho ya bidhaa na huduma za TTCL, kwenye Mkutano Mkuu wa 14
wa Wahandisi jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Mratibu wa Huduma Mpya za TTCL, Yonah Kulanga (wa kwanza
kushoto) akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi jijini Dar
es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) imesema inamajibu ya mawasiliano ya uhakika kwa
wahandisi wanaofanya kazi zao maeneo yasio na mawasiliano na sasa
imeanza kutoa huduma hiyo kwa wahandisi hao ili waweze kutekeleza kazi
zao kwa ufanisi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mhandisi Mratibu wa Huduma Mpya za TTCL, Yonah
Kulanga wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi jijini
Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo imewahakikishia wakandalasi hao kuwa
ipo tayari kusaidia kutoa mawasiliano hata maeneo yasio na mifumo ya
kawaida ya mawasiliano nchini.
Alisema
mawasiliano ni miongoni mwa nyenzo muhimu kwa makampuni hayo hivyo TTCL
inamajibu ya kutoa mawasiliano hata kwa maeneo ambayo hayana mfumo wa
mawasiliano wa kawaida kwa kufunga vifaa maalumu ambavyo vinasaidia
kampuni hizo kufanya mawasiliano yao wakiwa kwenye maeneo ya kazi.
Alisema
wahandisi wanafanya tafiti na mawasiliano nje na ndani ya nchi hivyo
kuhitaji mawasiliano ya uhakika wakati wote wawapo kazini. Aliongeza
kuwa wakandarasi wamekuwa wakifanya kazi maeneo ya porini sehemu ambazo
hazina mawasiliano ya mkongo, wala kopa na hata mawasiliano ya redio
jambo ambalo TTCL imeleta mapinduzi kwa wakandarasi hao ili kuweza
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na bila vikwazo vya mawasiliano.
"...Kwa
maeneo kama haya ambayo hayana mawasiliano TTCL tumekuja na majibu kwa
wahandisi katika maeneo kama haya tunaweza kuwapatia wahandisi
mawasiliano ya intaneti kwa kutumia mawasiliano ya sateliti, yaani
tunafunga vifaa maalumu vinavyo saidia kupata mawasiliano eneo
husika...," alisema Kulanga.
Alisema
kwa sasa maeneo yote ya Tanzania TTCL inaweza kutoa huduma hizo kwa
wahandisi watakao hitaji Aidha alisema huduma hii imesha tolewa, yataja
maeneo ambayo wamesha toa huduma hizo kuwa ni pamoja na Rukwa kwa baadhi
ya mbuga, Lindi Londo Forest, Mbuga ya Serengeti maeneo ya utafiti,
Kituo cha Tawiri, Kituo cha Utafiti Makutupora Dodoma, Maeneo ya Ufugaji
Kongwa, mbayo hayana mawasiliano kama wakanda.
Kwa
upande wake, Mhandisi wa Mkongo wa Taifa, Nsaji Mwamukonda alisema
wahandisi wanapewa fursa kubwa ya kutumia mkongo pamoja na faida zake
kwenye shughuli zao hivyo kuwataka pia kutumia kituo mahiri cha kutunzia
taarifa (Data Centre) kinachoendeshwa na TTCL katika kuhifadhi taarifa
zao kwa usalama.
Alisema
wahandisi wana taarifa muhimu ambavyo hutumika kwa shughuli mbalimbali
hivyo hazina budi kuhifadhiwa sehemu salama na ya uhakika hivyo kuwaomba
wajitokeze kukitumia kituo hicho cha kuhifadhi taarifa. "...Wahandisi
wetu wanataarifa muhimu katika kazi zao na nyingine wamekuwa
wakizitegemea kwenye tafiti hivyo nashauri makampuni haya kukitumia
kituo chetu kuhifadhi taarifa zao kiusalama," alisema Mwamukonda.
Mkutano
Mkuu wa 14 wa Wahandisi unafanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam
Septemba 1 na 2, 2016 katika viwanja vya Mlimani City ambapo makampuni
na taasisi mbalimbali wadau wa wahandisi ikiwemo TTCL zimeshiriki
kufanya maonesho juu ya huduma na bidhaa anuai kwa wajumbe kwenye
mkutano huo.
Post a Comment