Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bwana Fadhili Nkulu amewapa pole wahanga wa
moto uliotokea kwa hitilafu ya umeme na kusababisha hasara kubwa ambayo
hadi hivi sasa haijajulikana thamani ya vitu vilivyoungua kwa moto huo.
Tukio hilo limetokea majira ya Saa kumi na mbili jioni ambapo hitilafu hiyo ya umeme ilianzia katika nguzo ya umeme iliyopo katikati ya kiwanda hicho Majengo.
Katika hatua ya uzimwaji moto huo gari la serikali ilifika eneo la tukio Lakini halikufanikiwa kuuzima moto huo hadi uongozi wa serikali ulipoamua kuomba msaada wa gari kutoka kampuni ya madini ya accacia ndipo zoezi la uzimwa moto huo lilipo fanikiwa kwani Wilaya ya Kahama ina gari moja katika jeshi la Zima moto.
Mmoja wa mashuhuda na mhanga wa tukio hilo bw Enock Juma amesema kuwa hajaokoa kitu chochote ikiwa yeye ni mfanyakazi katika kiwanda hicho hata hivyo amesema anaiomba serikali kuwasaidia wahanga wa tukio hilo njia moja ama nyingine.

Post a Comment