SEHEMU YA KUMI NA TATU.
Yalikuwa maneno ya mwisho ndani ukurasa wa kijitabu
kile, maneno ambayo sasa yaliuponda sana moyo wangu, huku yakiniweka katika
hali nyingine, hali ambayo kwa mara ya kwanza nilikuwa sikuwahi kuijua kama
sababu ya kifo cha kaka yangu mpendwa, sababu ambazo mara kadhaa nilikuwa
nikimuuliza mama lakini hakuwahi hata siku moja kuniambia kilikuwa kimetokea
nini katika miaka kadhaa iliyokuwa imepita.
Ni kweli kaka Eddy aliamua kujitoa roho yake mwenyewe
yaani kunyinyonga kutoka na mapenzi, hakika alikuwa amependa sana, katika namna
ya ajabu sana mpaka kufikia maamuzi yale, ambayo mwanzoni ilibaki kuwa siri
ambayo si kuwa naitambua.
Ni kiwa kitandani pale nilianza kutoa shutuma
kali kwa Irene kama vile nilikuwa nimewahi kumwona, nikiamini moja kwa moja
yeye ndio sababu ya kifo kile. Na kama alikuwa hampendi kaka kwanini alikubali
kuwa nae?, hakika nilijiuliza maswali ambayo yalizidi kuongeza gadhabu katika
mwili wangu.
Sasa kitanda kilikuwa mwiba mkali, mwiba
unachoma katika kila pande za mwili wangu, sikutamani kuendelea kuwa juu yake,
niliamua kujitoa na kuelekea nje ya chumba changu. Wakati huo kutoka kwangu
nilikaribisha na harufu nzuri ya chakula. Huku tabasamu pana la mama likinikaribisha,
kabla ya kuniambia ya kuwa muda si mrefu alikuwa akitaka kuja kunigongea
iliniweze kupata chakula. Ni kama vile nilikuwa nimeota kutoka kwangu kwa muda
ule. Na mimi sikutaka kuonesha tofauti yoyote niliachia tabasamu liliojaa
upendo kwa mama yangu.
________
Siku ilikuwa tofauti sana, mara nyingi huwa
mama anachelewa kula lakini siku hiyo tulijumuhika pamoja katika meza ya
chakula, huku akiyatawala maongezi muda wote wa chakula, maongezi ambayo yalinipa
faraja sana na hata kusahau machungu ambayo yalikuwa yamejenga ndani ya mwili
wangu. Nilikula sana tofauti hata na kawaida, na kama ilivyo kwenye upande wa
kupika mama hakuwahi kuniangusha hata kidogo. Chakula kilikuwa kitamu haswa,
kadri nilivyokuwa naona kama naridhika kula lakini utamu wa chakula kile,
ulinifanya niendelee kula tu.
Hatimaye tumbo langu lilionekana kuzidiwa na
hali ya kuendelea kula hivyo niliona wazi ningesabisha raha kuwa karaha muda
wowote. Zoezi la kula lilinishinda huku nikimuahidi mama ya kuwa kesho asabuhi
ningekiamkia chakula kile mapema sana, nilikuwa nikiogea katika hali ambayo
ilifanya mama kutoka na kicheko kizito tukiwa pale, huku akinichombeza na
maneno ya utani kama kawaida yake.
Tuliendelea kukaa mezani pale kwa muda kidogo
baada ya kuamaliza kula. Hatimaye mama aliniaga kulekea chumbani kwake,
niliamua kukaa pale sebuleni kwa muda kidogo huku nikitazama runinga, kidogo iliweza
kunipotezea mawazo yalikuwa yanapita kichwani mwangu, kiukweli nilikuwa na
mawazo kadhaa wa kadhaa ya kinitawala kichwani mwangu japo nilijaribu kupambana
nayo kiume lakini yalionekana kuniandama sana.
Runinga nayo ilionekana kushindwa kupambana
na mawazo yangu, ambayo kiasi kikubwa nilikuwa nikifikiria kuhusu kaka, ni
kweli alikuwa amepotea katika kifo ambacho kwa mtu wa kawaida unaweza ukadhani
ni cha kizembe lakini kwa upande wangu niliumia mno.
Niliamua kuingia chumbani kwangu, kwa wakati
huo muda ulikuwa umeenda sana, kutokana na uchovu wa mawazo yalikuwa
yakinitawala nilivyoweka tu mwili wangu juu ya kitanda, usingizi wa aina yake
ulikuja kunichukua.
Na kunifikisha asubuhi ambayo ilianza kwa
kupendeza sana machoni wangu, hakika kama ilivyoanza kwa kupendeza, siku ilisha
kwa kupendeza pia kwa upande wetu.
Niliendelea kukaa nyumbani, siku nazo
hazikuchelewa hatimaye likizo yangu iliisha na kurejea shuleni wakati wote mama
hakuwahi kuniambia chochote kuhusu kaka Eddy juu ya siri na mimi sikutaka
kumgasi niliamini wazi tayari nilikuwa nimeshafahamu hiyo siri ambayo mama
allikuwa akitaka kuniambia, hivyo sikutaka kujishungulisha sana.
Nilirejea shule ikiwa imebakiza miezi michache
ilituweze kufanya mtihani wangu wa mwisho. Taratibu nilianza kupoteza habari za
kaka Eddy, siku zilivyokuwa zinaenda shuleni pale. Nilijua juu ya kufikiri
suala kama lile lingiweza kunipotezea katika masomo yangu. Japo mwazoni ilikuwa
ngumu lakini kutokana na jambo ambalo lilikuwa linanikabili, mbeleni mambo yale
yalianza kupotea. Huku nikiendelee kupambana sana katika kuipigania Elimu yangu
kwa kiasi kikubwa.
Ikiwa imebaki wiki tatu kabla ya kufanya
mtihani, katika mchana moja. Nikiwa na tafakari ya kile nilichokuwa nimekisoma
ndani ya siku hiyo. Nilishangaa tu nikipewa taarifa na moja ya mwanafunzi
mwenzangu ambaye tulikuwa tumezoena sana. Taarifa iliyokuwa ikinihitaji
kuelekea ofisini kuona na mwalimu Rajabu omary, ambaye tulikuwa tumezoena sana
kutokana na kufanya vizuri sana katika somo lake la historia. Sikujua sababu ya
wito katika namna moja ama nyingine lakini siku hiyo ilionekana tofauti.
Nilivuta pumzi ndefu huku akili yangu
ikijenga hofu ndani yake. Ni hiyo hofu ambayo sikujua kama ingeleta machungu
sana katika mwili wangu na kuongeza uchungu maradufu juu ya viumbe viitwavyo
wanawake, uchungu ambao kwa muda mwingi ulikuwa umeshapotea na kusaulika kabisa
ndani ya mwili wangu.
Nikiwa ndani ya hali ya sintofahamu, miguu
yangu iliongoza kuelekea ofisini, katika moja ya ofisi ambayo kichwa changu,
kilikuwa kinaongoza miguu vilivyo, hatimaye nilikaribisha na ukimya wa hali ya
juu, ukimya ambao ulitokana na kutokuwepo walimu wengi ndani ya ofisi ile, huku
wachache wakionekana kuwa bize na shunguli zao. Ilinibidi nielekea moja kwa
moja katika meza ya mwalimu Rajabu. Ambaye alinikaribisha katika namna ambayo,
nilianza kuhisi uwenda kunajambo zito lipo ndani yake, ambalo kwa kiasi kikubwa
lilikuwa linanihusu mimi haswa. Fikra zangu zikaanza kupambana na muonekano ule
wa mwalimu Rajabu, huku nikiomba kusiwe na jambo baya lolote ambalo lingeniweka
katika hali ambayo sikuwahi kuitegemea.
Ni kweli mwalimu Rajabu alikuwa ana jambo
zito ambalo lilikuwa likinihusu sana.
Post a Comment