Waziri wa
habari Sudan Kusini amesema kuwa serikali haitajibu madai ya ripoti
mpya inayodai kuwa viongozi wa nchi hiyo wananufaika kutokana na vita
vya wenyewe kwa wenyewe vinayoendelea nchini humo.
Michael
Maquei Lueth amesema kuwa serikali ina mambo mengi ya kusema kuhusu
madai hayo lakini itafanya hivyo ikiwa itapatiwa rasmi taarifa za kina.
Ripoti
iliyosimamiwa na muigizaji wa Hollywood na mwanakampeni George Clooney
inadai kuwa Rais Salva Kiir,kiongozi wa upinzani Riek Machar na mkuu wa
jeshi pamoja na familia zao wanafaida zinazofanana.
Inawaunganisha
wasomi wa Sudan Kusini katika mchezo wa fedha unaojumuisha nyumba za
kifahari, migodi ,mafuta na kampuni nyengine.
Vita hivyo vilivyoanza 2013 vimedhoofisha uchumi wa nchi
Post a Comment