0


WATU wawili ambao ni mkufunzi na mwanafunzi wake wamejeruhiwa vibaya baada ya ndege waliokuwa wakifanyia mazoezi kuanguka  jijini Nairobi nchini Kenya leo asubuhi Jumatatu, Septemba 12.

Taarifa ya polisi jijini Nairobi imeeleza kuwa mkufunzi na mwanafunzi wake walikuwa kwenye ndege hiyo wakifanya kutoka Uwanja wa Ndege wa Wilson Airport, ndege hiyo ilianguka kwenye shamba la mahindi lililopo katika eneo la Kibiku, Ngong jijini humo.

Polisi walifika eneo la tukio na kuwaokoa majeruhi hao kisha kuwakimbiza hospitali kwa ajili ya matibabu huku mamlaka husika zikiendelea na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo.

Tukio hilo limekja ikiwa ni siku chache tu baada ya ndege mpya helikopta ya polisi aina ya Agusta Westland 139 kuanguka na kujeruhi maofisa wanne katika eneo la Mathare Kaskazini A, Nairobi.

Alhamisi, September 8, mwanamke mmoja alifariki dunia na wengine watano kujeuhiwa vibaya ambapo ndege ndogo ilianguka kwenye moto na kuteketea mjini Naivasha nchini humo.

Post a Comment

 
Top