0
 Kiongozi wa waasi jamil Mukulu
Kiongozi wa waasi jamil Mukulu
Kiongozi wa waasi nchini Uganda atazuiliwa kwa miezi 14 katika gereza la Luzira mjini Kampala baada ya kushtakiwa na shtaka la uhaini na mauaji,kulingana na gazeti la Daily Monitor nchini humo.
Jamil Mukulu alikamatwa nchini Tanzania mwaka uliopita baada ya kutoroka kwa zaidi ya muongo mmoja.
Bwana Mukulu anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi la Allied Democratic Forces,kundi la waasi linalotekeleza operesheni zake kati ya mashariki mwa DRC na Uganda tangu mwaka 1990.
Serikali ya Uganda imelishtumu kundi lake kwa mauaji ya viongozi wa kidini mwaka 2014.
Pia imelishtumu kundi hilo kwa kupanga njama za kuipindua serikali.
Bwana Mukulu anadaiwa kushirikiana na makundi ya kigaidi ya kimataifa na aliorodheshwa katika orodha ya Umoja wa Mataifa mwaka 2011 kwa kujaribu kudhoofisha DRC.

Post a Comment

 
Top