0

Baada ya ndege mpya mbili za Air Tanzania zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwasili nchini  Leo September 28 2016 umefanyika uzinduzi wa Ndege hizo aina ya Bombadier Q400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Dar es salaam na mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Rais Magufli alipopata nafasi ya kuhutubia alizungumza mambo haya
 'ATCL lilikuwa linajiendesha si kiueledi, lilikuwa limebweteka, wafanyakazi wanafanya kazi kimazoea'-
 'Ukitumia ndege za Jet kwenda Songea mafuta ni mil 28.9, lakini ndege hizi mafuta ni milioni 1 kama utaenda Songea'
 'Tulianza na kulipa 40% na walipomaliza tulimalizia 60% na tuna mpango wa kununua ndege nyingine 2 kubwa na fedha zipo'-JPM 
 'Wengine ndege hizi wamenunua kwa bei kubwa lakini sisi wenye Cash tumenunua kwa bei ya chini'

Post a Comment

 
Top