WATANZANIA 12 jana wametekwa katika eneo la Namoyo, Jimbo la Kivu Kusini
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) na kikundi cha waasi cha
Maimai, anaandika Aisha Amran.
Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa watu hao ni madereva wa malori na kwamba, baada ya kutekwa wakiwa katika magari yao, walishushwa na kupelekwa porini na kisha malori yao manne kuteketezwa kwa moto.
Kati ya malori hayo, nane yanamilikiwa na mfanyabiashara wa kitanzania,
Azim Dewji na mengine ni ya wafanyabiashara kutoka Kenya.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, waasi hao wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10
jioni kwamba walipwe fedha kiasi cha Dola za kimarekani 4,000 (zaidi ya
milioni Sh. Milioni 8 za Tanzania) kwa kila dereva ili waweze kuwaachia
mateka hao.
“Wametishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha
wanachokitaka itakapofika saa 10 jioni leo ingawa katika tukio hilo
madereva wawili wa kitanzania, wamefanikiwa kutoroka ambao ndiyo
waliosaidia kutoa taarifa rasmi,” imeeleza taarifa hiyo.
Serikali ya Tanzania imedai kuwa, tayari imechukua hatua za awali za
kuwasiliana na serikali ya DRC ili kuhakikisha kuwa madereva hao
wanaachiwa kwa haraka iwezekanavyo wakiwa salama.
Hata hivyo serikali haijafafanua kuwa, ni hatua gani zimechukuliwa ili
kuwaokoa madereva hao, kama ni kulipa kiasi cha fedha kinachohitajika au
la.
Tukio hili ni la pili kutokea katika miaka ya hivi karibuni ambapo mwaka
2015 Mashekhe kutoka Tanzania walitekwa nchini DRC, lakini walifanikiwa
kuachiwa huru bila madhara yoyote.
Post a Comment