Baraza la Senete la Bunge la brazil limepiga kura ya kumwondoa
madarakani rais Dilma Rouseff na hivyo kuhitimisha utawala wa miaka 13
wa chama cha mrengo wa kushoto cha workers Party.
Upinzani ulihitaji kura 54 miongoni mwa 81 za maseneta ili
kumtimua Rouseff. Hata hiyo ulipata zaidi ya kura ulizotazamia baada ya
ushindi mkubwa wa kura 61 dhidi ya 20.
Kundolewa kwa Rouseff sasa kunazua maswali mengi yasiyoweza
kupata majibu kwa urahisi. Michel Temer ambae ni makamu wake, atahudumu
muhula uliosalia hadi mwaka 2018 wakati wa kufanyika uchaguzi mkuu.Hata
hivyo wabrazil tayari hameonyesha kutoridhika na utawala wake.
Mwezi Mei baada ya kuteuliwa rais wa muda kufuatia kusimamishwa kazi Rouseff na Senete,mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 75 aliwatagaza mawaziri wake ambao wote ni wazungu, swala lilokashifiwa vikali, katika taifa hilo lilo na zaidi ya asilimia 50 ya watu wasiokuwa wazungu.
Mawaziri wake watatu walilazimika kujizulu wiki kadhaa baada ya kuanza kazi ,kutokana na kuhusishwa na rushwa,ambayo pia anamuandama Tremer. Washirika wa Rouseff wamesema watawasilisha rufaa katika mahakama ya juu ya nchi hiyo kupiga uamuzi huo.Mapema kabla ya kufanyika kura hiyo usalama ulimarishwa karibu na majengo ya baraza hilo la senete huku hali hiyo ikichangia msongamano mkubwa wa magari.
Rouseff kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha workers party
anatuhumiwa kwa udanganyifu wa fedha za bajeti muda mfupi kabla ya
uchaguzi wa mwaka wa 2014 ili kuficha hali mbaya ya kiuchumi inayokabili
taifa hilo,tuhuma alizokanusha vikali. Wakati akimtetea katika baraza
la senete wakili wake Jose Eduardo Cardozo alimwondoa lawamani mteja
wake."Kama kuna mtu aliyesahihi na msafi katika mfumo wa kisiasa wa
Brazil uliokithiri rushwa ,ni Dilma Rouseff. Yeye havumilii rushwa,hata
kamwe. Hajahusika kwa vyoyote katika ulaji rushwa, au hata kutuhumiwa"
alisema Cardozo
Wachanganuzi wengi wa kisiasa walikuwa tayari wametabiri
kuondolewa madarakani Rouseff. Chama chake cha workers party ambacho
kimeongoza kwa zaidi ya mwongo mmoja nchini Brazil kimewaondoa watu
millioni 29 katika lindi la umaskini.
Post a Comment