Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Mchemba amevitaka Vyombo vya
ulinzi na usalama mkoani Lindi na Mtwara kuimarisha ulinzi
kwenye maeneo ya bahari na
kuwatega kuwakamata watu
wote wanaotumia bandari bubu kupitishia
magendo pamoja na
madawa ya kulevya
Agizo hilo amelitoa wakati
alipokuwa anazungumza na vikosi
vya ulinzi na usalama mkoani hapa
kwenye ziara yake ya kikazi ya
siku moja
Mchemba alisema kuwa mkoa wa Lindi una changamoto nyingi ikiwemo bandari bubu na uwepo wa hali hiyo ume sababisha
upitishaji wa madawa ya kulevya na
bidhaa za magendo na
kupelekea kukwepa kodi
Alisema niwajibu wa
vyombo vya ulinzi kuhakikisha vinapamnana na wanakamatwa watu wote
wanaojiusisha na shughuli hiyo pia zoezi hilo linatakiwa kuwa endelevu kwa hatima ya
vijana na maslai pana ya taifa.
Mchemba aliongeza kwa kusema
suala la ulinzi na usalama
halina mjadala hivyo kila mtanzania
anawajibu wa kulinda amani na mtu yoyote atakaye diriki kuchezea amani ya nchi
hatakuwa ni adui wa wa wote hataweza kuvumiliwa
Awali akitoa taarifa
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ya mkoa mkuu wa
mkoa wa Lindi Godfrey Zambi
alisema mkoa wa Lindi unachangamoto nyingi za
kiulinzi ikiwemo kuwepo kwa wakimbizi 1892 waliotoka
nchi Msumbuji ambao urai
wao hawatambuliki hadi sasa.
Zambi alimuomba wa
Waziri huyo wa mambo
ya ndani kuwatambua wakimbizi hao kwa kuwapa uraia wa kudumu kama
watanzania au kuwarudisha kwao
ili wakaendeleze nchi yao.
VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI LINDI VIKIMSIKILIZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU MCHEMBA
Post a Comment