Naibu waziri wa Maliasili na
Utalii Injinia Ramo Makani amesema wizara imejipanga kuboresha na kuimarisha vivutio vya vya utalii
wa ndani ikiwemo Mali kale na
fukwe za bahari na hoteli za kitalii ili kuongeza pato la taifa
Hayo aliyasema juzi
wakati alipokuwa anazungumza na wa
wananchi wa vijiji vya Mtoni wilaya
Kilwa na Kijiweni wilaya ya
Lindi kwenye ziara yake ya
kikazi ya siku moja mkoani Lindi
Makini Alisema ili
kutumia vizuri fursa za maliasili zilizopo nchini katika kukuza uchumi wa taifa serikali haina budi
kuboresha huduma hizo ili iweze kuleta tija kwa kuchangia pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi yetu
“ipo sababu ya kuongeza
nguvu katika sekta ya utalii
na maliasili ili iwe miongoni mwa sekta zinazotumainiwa nchini
kwa kuongeza pato la taifa
hatimaye kukuza uchumi wa Taifa “ alisema Makani.
alisema kuwa Wizara inalengo la kuboresha miundombinu ya vivutio vya ndani na kulinda
na kuhifadhi na mazingira ili, kuboresha
utoaji wahuduma pamoja na kuendeleza vivutio vilivyopo na kuanzisha vivutio
vipya.
Injinia Makani alisema
utalii wa ndani ukiimarishwa utaweza kuongeza mapato ambayo yataweza kuwa sawa
na mapato yanayotokana na
watalii wa nje kwani jamii kwa
sasa ina mwamko mkubwa wa kutembelea
vivutio vilivyopo hapa nchini.
Aidha naibu waziri
amewataka wananchi
wanaoishindi kando kando ya
ufukwe wa bahari hindi kutorubuniwa na
matajiri na kuanza kuuza
maeneo yao ovyo badala yake
kuendelea kuulinda
Kwa upande wa Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kilwa Zablon Bugingo
alisema kuwa halmashauri ya wilaya
Kilwa imeanza mikakati ya
kuboresha kwa kufanya ukarabati Magofu ya
zamani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili yaweze kuingiza mapato
Post a Comment