0
 WANAFUNZI wa shule ya sekondari  Rondo Mtene wakiwa  hospitali  baada ya  kupata ajali kijiji cha Rutamba  wakielekea  kwenye  maonesho ya  Nanenane  Ngongo Lindi
 Mkuu  wa mkoa wa Lindi Godfrey  Zambi akizungumza  na wanafunzi  waliopata ajali ambao  walilazwa katika   Hospitali ya sokoini  wakati alipotembelea  hospitali hiyo

 Mkuu  wa mkoa wa Lindi Godfrey  Zambi akizungumza  na wanafunzi  waliopata ajali ambao  walilazwa katika   Hospitali ya sokoini  wakati alipotembelea  hospitali hiyo.


Wanafunzi  90  wa shule ya Sekondari Mnara  Rondo  Jimbo la Mtama Lindi wamenusurika kufa baada ya Lorry walilokuwa wakisafiria kuelekea kwenye Maonesho  ya  nanane  Ngongo   kupinduka  na  kikatika bomba.
 
Akizungumzia tukio  Mwalimu  Maulidi  Imili alisema   Tukio  hilo  lilitokea  majira  ya  saa  tano  katika  kijiji  cha Rutamba wakati  alipokuwa wanatoka  Shule ya Sekondari  Mnara  akiwa na  wanafunzi 90 wakiokuwa  wanaelekea   kwenye  maonosho ya  Nanenane  kujifuza mamboa  mbalimbali.
 
Maulidi  alisema  baada ya  kufika eneo  kijiji  cha  Rutamba  dereva alikuwa anakwepa  Korongo  gari  ikayumba  kulia na  kushoto  ndipo  bomba  walizokuwa  wameshikiria  zikakatika  na kuwamwaga  chini.
 
  Kwa upande wake  kaimu  mganga  mkuu  wa hospitali ya  sokoine  Msafiri  Rignald  mekiri kupokea  wanafunzi   majerui  10  ambao  kati hayo  wanne  hali zao  mbaya kutokana  na  kupata   kuvujika , mguu  kiuno.
 
 Kamanda wa  polisi  Renata  Mzinga amethibitisha kutokea  kwa  tukio hilo na  kueleza kuwa wanafunzi 80 kati ya waliopata ajili  hawakuumia  na  10  wanaendelea  kupata  matibabu katika  hospitali ya  Mkoa ya Sokoin.
 
Wakati  huyo  Mkuu wa  mkoa wa Lindi Godfrey Zambi  ameuagiza  uongozi  wa  hospitali  ya Rufaa  Sokoini  kuzingatia  maadili ya  kazi  yao ikiwemo  kuhudumia  wagonjwa  na kufanya usafi  kwenye  maeneo yao.
 
Agizo hilo  amelitoa   wakati  alipowatembelea  hospitali  hapo  kuwaona  wanafunzi wa shule ya  sekondari Mnara waliopata ajali  baada ya  gari yao kupinduka  wakielekea  kwenye  maonesho ya sabasaba.
 
Zambi  amesikitishwa  na kitendo cha  wanafunzi waliopata  ajili   kukosa  matibabu  kwa zaidi ya  masaa  saba   baada ya  kufika  katika  hospitali hiy.
 
Alisema  kitendo cha  wafanyakazi wa  hospitali  kutowajali  wateja  ni  kukiuka  maadili ya idara ya  idara ya afya  na kinakatisha  tamaa wagonjwa kupona na wakati mwingine kusababisha   vifo kwa  wagonjwa.
 
Akizungumzia  mapungufu  hayo  kaimu  mganga  mkuu Msafiri  Regnald alisema wanafunzi hao wamechelewa kupata  matibabu  kutokana  na upungufu  wa madaktari  kwani hospitali hiyo  ina  Daktari mmoja ambay  kwa   muda  huyo  alikuwa anahudumia   wangonjwa  wodi  nyingine

Post a Comment

 
Top